}

HIZI NDIO SABABU NCHI ZA AFRIKA KUSHINDWA KIUCHUMI.

Na. Happy Shirima.

NCHI za Afrika zimekuwa zikishindwa kukua kiuchumi kutokana na kutoa kipaumbele kwa misamaha ya Kodi kwa makampuni ya kibiashara haswa yale ya nje pamoja ukwepaji kodi na utoroshaji wa fedha kutoka Afrika na kwenda kuzificha nchi za nje ikiwemo Uswisi na Iland.

Mapema leo hii, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam  Prof Prosper Ngowi, wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha mzumbe alipokua katika  mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya policy forum wa uwasilishwaji wa kitabu kilichoandikwa kwa ushirikiano wa nchi ya Norway na chuo kikuu cha mzumbe kuhusu usiri wa kodi za kimataifa na utoroshaji wa mitaji kutoka Afrika.

Aidha Prof Ngowi amesema kuwa, uwekezaji  unahitaji mazingira rafiki, wezeshi na ya kutabirika ikiwemo  miundombinu bora ya barabara, viwanja vya ndege, reli pamoja na sera nzuri  na nguvu kazi ya kutosha kwenye taifa na kutokuwepo kwa vitendo vya ubadhilifu haswa rushwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Umoja wa mataifa  unatakiwa kuingilia kati utoroshwaji wa fedha zinazopelekwa  nchi za ulaya hasusani nchi ya  Uswisi kwani kunachangia ongezeko la fedha haramu zinazotokana na ukwepaji Kodi na biashara haramu kutokana na kuwa nchi za Afrika pekee hasa  Tanzania haziwezi kukabiliana na tatizo hilo.

Ukwepaji kodi umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya nchi huku Serekali ikishindwa kutoa huduma muhimu kwa umma ikiwemo elimu bora,  Afya, upatikanaji wa maji ujenzi wa miundombinu pamoja na ulinzi na usalama wa raia wake hivyo elimu kuhusu ulipaji kodi iongezwe zaidi pamoja na ushirikishwaji wa viongozi wa dini ili kuweka hofu ya Mungu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.