}

FAMILIA ILIYODHURUMIWA KIWANJA KARIAKOO YAMUANGUKIA RAIS JPM.

Na. Happy Shirima.
FAMILIA ya Mzee Maulid Tosiri imemuomba Rais John Magufuli kuisaidia familia hiyo, ili kuweza kupata haki yao ya kiwanja kilichopo mtaa wa ukami plot no 11 Block 70 kariakoo Manispaa ya ilala kilichozulumiwa na Bi Hafsa Machano ambae anadai anakimiliki kihali kiwanja hicho.

Mapema leo hii, akizungumza  na wanahabari  msemaji wa familia hiyo, Iddi Maulid amesema kuwa,wamekuwa wakifatilia kupatikana kwa haki yao kwa ukaribu zaidi kwa kuwashirikisha viongozi mbali mbali lakini hawajapata mafanikio yoyote.

"Ni muda mrefu sasa tangu tulipozulumiwa haki ya mzee wetu Iddi Tosiri , tumekuwa tukituma barua za kuomba msaada kwa viongozi mbalimbali ndani ya Serikali ikiwemo mkuu wa Wilaya ,Mkoa, kamishna wa ardhi pamoja ofisi ya Waziri Mkuu "amesema Iddi.

 Amesema kuwa,kiwanja hicho kilikua kinamilikiwa na Mzee Iddi Tosiri kwa miaka 28 hadi pale alipotokea mwekezaji wa kutaka kuingia nae ubia wa kujenga gorofa moja ndipo alipoamua kumpa documenti Wakili Salum Macho kwa ajili ya kutengeza ubia baina mzee huyo na Said Rabai.

"Wakili Machano alipatiwa document za hati ya 99 na mzee Iddi kwa ajili ya kutengeza ubia wa kujenga gorofa lakini alichokifanya ni kummilikisha mali ile Mke wake ambae ni Bi Hafsa Machano kwa madai ya kuwa eneo hilo ameuziwa na Serikali.

Aidha amesema kuwa, ana imani na Serikali iliyopo madarakani kwa sasa watafanikiwa kupata haki yao kutokana na Rais John Magufuli anaguswa na kutetea wanyonge pamoja na kuwatatulia shida zao kutokana na changamoto zinazowakabili wananchi wake.

 Hata hivyo, amesema mzee Iddi alinunua kiwanja hicho mahakamani kwa sh elf 5 , ambayo ilikuwa ni mali ya ndugu watatu na kudai kuwa vielelezo vyote wanavyo lakini wakili Salum Machano alimgeuka na kummilikisha Mke wake bi Hafsa Salum na yeye alipoona anaelekea kushindwa aliamua kumpa kesi aliekuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya awamu ya nne Mustafa Mkulo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.