}

MKURUGENZI SAUTI ZA BUSARA, WADAU TUMIENI FURSA KUPITIA TAMASHA LA BUSARA.

Na. Happy Shirima.

Wadau mbalimbali na wafanyabiashara nchini wametakiwa kutumia frusa zinazopatikana kupitia Tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukuza uchumi pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.

Mapema Leo hii akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema kuwa, Tamasha hilo litafanyika Mji Mkongwe Visiwani Zanzibar February 8 hadi 11 ambapo  limedhaminiwa na ubalozi wa Uholanzi na Norway.

 Aidha ameongeza kuwa Tamasha hilo linalofanyika kwa mara ya 15 litawahusisha   wasanii zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Ikiwemo Morocco, Afrika kusini, Uganda Dermark,  na wenyeji Tanzania.

Amesema tamasha hilo litakuwa na maonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa asilimia 100 yatapigwa mubashara huku orodha ya wanamuziki ikijitoshereza katika nyanja nyingi, ikijumuisha sauti maridhawa kutoka Zanzibar na Tanzania bara, pamoja na vikundi 15 vilivyojiandaa kuionyesha dunia muziki tofauti wenye hasili ya nyumbani.

 Kwa upande wa mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo kutoka Tanzania ni pamoja na msanii Mkongwe saida karoli ambapo amesema kuwa tamasha hilo lina lengo nzuri kwani linawakutanisha pamoja wasanii kutoka sehemu mbalimbali za afrika na duniani kote.

Amesema hii ni mara ya pili kwake kushiriki katika tamasha hilo ambapo alishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutoa  shukrani zake kwa  waandaaji wa tamasha hilo kwani  litazidi kuwatakutanisha wasanii pamoja na kukuza vipaji vyao.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.