}

WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018

Waziri wa Mifugo na uvuvi Mh.Luaga Mpina (Katikati)  akizungumza jambo alipotembelea Ranchi ya mifugo ya Uvinza. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina  ameutaka uongozi wa  Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS)  kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo  ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu  tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na  Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO)kabla ya Selikali kuwatoa kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.

Waziri Mpina  amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa  Philemoni Wambura  kuwaandikia  barua  ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40  na kwamba wawekezaji ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari mosi mwakani.

Awali, Meneja wa (TGTS)   Audax Kalulama  akizungumza kwa simu  na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema kwamba  eneo hilo wanamiliki  kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na Wizara  ya Mifugo kuonyesha  taarifa  za umiliki wa eneo hilo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.