}

RUSHWA YA NGONO YANUKA MASHULENI, HOSPITALI, POLISI, MAHAKAMANI NA SEKTA BINAFSI.

Na. Happy Shirima.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya rufaa Engera Kileo akizungumza wakati alipokua katika jukwaa la  siku 16 ya upingaji wa ukatili wa jinsia jijini Dar es salsam.
Tatizo la Rushwa ya ngono bado nichangamato hapa nchini haswa kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Hospitali, Vyuoni, Shule, Polisi, Mahakamani pamoja na Sekta binafsi jambo ambalo linapelekea kurudisha nyuma harakati za utendaji bora wa kazi na maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mapema leo hii, Jaji Mtaafu wa Mahakama ya Rufaan Engera Kileo wakati alipokua katika jukwaa la  siku 16 ya upingaji wa ukatili wa jinsia yaliodhaminiwa na Shirikia la Women Fund Tanzania (WFT) ambapo wamelenga kutoa elimu na kuhamasisha Taasisi za elimu ya juu.

Amesema tatizo la rushwa ya ngono bado linahitaji kupingwa na kila mtu kwani linakwamisha harakati za maendeleo pamoja nakupelekea athari kubwa ndani ya jamii ikiwemo kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya ukimwi, huku akiomba sheria hiyo ifanyiwe marekebisho kwa upande wa rushwa ya ngono kwani adhabu yake ni ndogo ukilinganisha na madhara anayopata mlalamikaji. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania  Mary Rusimbi amesema lengo la mjadala huo ni kueneza vita ya kupinga Rushwa ya ngono kupitia kampeni ya 'Vunja ukimya, Rushwa ya ngono inadhalilisha na inaua' ili kuleta mabadiliko katika jamii na kujenga makubaliano ya pamoja na jinsi ya kusambaza kampeni hiyo.

Amesema kuwa, wanafunzi wana nafasi kubwa katika kusambaza kampeni hiyo ambayo wanategemea kupata mabadiliko chanya kwa kuvunja ukimya juu ya matendo ya rushwa ya ngono wanayofanyiwa huko mashuleni na vyuoni.

Hata hivyo amewaomba wanafunzi wawe wazi juu ya wanayofanyiwa na walimu wao kwani sheria ya rushwa ipo na inafanya kazi hivyo ni vyema kuripoti kila wanapofanyiwa vitendo vya kudhalilisha na kuwa mabalozi wazuri kwa Jamii na kizazi kijacho kwenye vita dhidi ya rushwa ya ngono.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.