}

RC GODFREY ZAMBI WA LINDI AANDAA BONANZA LA TISA DESEMBA.

Na. Geofrey Jacka-Lindi.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh.Godfrey Zambi(Aliyesimama)akizungumza Karina bonanza la michezo aliloliandaa uwanja wa Ilulu Lindi. 

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi amewaongoza wakazi wa Lindi kuadhimisha Siku ya uhuru wa Tanzania kwakuandaa bonanza La michezo mbalimbali.
Akizungumza Katika bonanza hilo Zambi amesema, wananchi washerehekee wakiwa na kumbukumbu yakupeleka watoto shule Huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii Kama kaulimbiu ya Mh. Rais Magufuli inavyosema.

"Mkoa wetu bado upo chini Sana Katika elimu, hivyo nashauri tuwapeleke vijana wetu shule kwa Wale waliofaulu darasa la Saba, lakini pia mwezi Januari tuwapeleke watoto kuanza darasa la Kwanza kwa wingi"

Akizungumzia zao la korosho Zambi amesema, minada imeenda vizuri na sasa unaelekea kufanyika mnada wa Saba Katika msimu huu, huku akisema wakulima wanaendelea kunufaika na zao hilo kutokana na bei kuwa ni yakuridhisha.

Bonanza la mkuu wa mkoa limekutanisha timu mbalimbali ikiwamo Magereza, Polisi, timu ya wilaya ya Kilwa na Nachingwea pamoja na timu nyingine nyingi zilizoandaliwa na wananchi wenyewe. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.