}

TIMU YA MAGEREZA LINDI YAWA TISHIO BONANZA LA MKUU WA MKOA TISA DESEMBA.

Na. Geofrey Jacka -Lindi.
Timu ya Mpira wa miguu ya Jeshi La Magereza mkoani Lindi, imezidi kuwa tishio kwenye bonanza La tisa desemba lililoandaliwa na mkuu wa mkoa Mh.Godfrey Zambi

Magereza imedhihirisha umahili wake baada yakuitandika timu ya Wilaya ya Kilwa goli nne kwa moja huku goli tatu zikifungwa kwa mikwaju ya penati.

Mikwaju ya penati ilipigwa baada ya timu hizo kutoka sare ya Moja kwa Moja kitu kilichopelekea Magereza kushinda penati tatu huku Kilwa wakipoteza penati tatu ambazo golikipa Davis Sabayo alifanikiwa kuzidaka.

Nahodha wa Magereza ambaye pia ni golikipa Davis Sabayo amejigamba nakusema kuwa mazoezi yamewasaidia mana haamini uchawi kwenye Mpira wa miguu.
"Nafurahi nimeweza kudaka penati nakuwezesha Magereza kushinda,  ni mazoezi tuu yamesaidia hakuna uchawi" alisema Sabayo. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.