}

DC-NACHINGWEA RUKIA MUWANGO AISINDIKIZA TIMU YAKE BONANZA LA TISA DESEMBA.

Na. Geofrey Jacka-Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mh.Rukia Muwango akifuatilia michezo ya bonanza La Tisa Desemba Katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi. 
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mh.Rukia Muwango ameisindikiza timu ya wilaya yake kushiriki bonanza La miaka 56 ya uhuru wa Tanzania lililoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi.
Katika kuheshimu uwepo wa mkuu wao wa wilaya, vijana wa timu ya wilaya ya Nachingwea wameipiga timu ya Lindi vijijini goli Moja lililopelekea kuingia nusu fainali Katika bonanza hilo.

Licha ya mvua kubwa kunyesha mkoani Lindi Leo hii lakini bonanza linaendelea Huku timu za michezo mbalimbali zikiendelea kuoneshana uwezo mbele ya mkuu wa mkoa.

Michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, Mpira wa wavu, kufukuza na mingine mingi, huku msafara wa bodaboda ukisindikizwa na polisi uliingia uwanjani kwa vifijo nakupelekea Sherehe za uhuru mkoani Lindi kufana.





No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.