}

WAZIRI JAFO WA TAMISEMI AMPA WIKI SITA MKANDARASI WA MAJI KUANZA KUTOA HUDUMA.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amemtaka mkandarasi wa mradi wa maji katika eneo la Kivindo Wilayani Muheza kukamilisha mradi huo na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ndani ya wiki sita.

Akikagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali wilaya muheza Mh.Jaffo amesema mradi huo umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake ambapo mkandarasi umeahidi kuwa ataukamilisha ndani ya  wiki sita kuanzia sasa.

Mh.Jafo amefanikiwa kutembelea Miradi ya afya na elimu katika kituo cha afya Mkuzi na Ubwari na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kilulu na kuwapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikia katika miradi hiyo. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.