}

DC-KISARE WA UBUNGO AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI MAPAMBANO UKATILI WA KIJINSIA.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Makoli amewataka wananchi kushiriki kikamlifu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia unaoendelea kujitokeza katika jamii.

Akifungua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Jijini Dar es salaam Mh.Makoli amesema kauli mbiu inasema Funguka ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumwachi mtu salama ambayo inasisitiza agenda ya dunia ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu kwa makundi yaliyosahaulika. 

Mh. Makoli amesema athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa katika nyanja ya kisiasa,kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ambapo inaonyesha kuwa wanawake wa 4 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Kwaupande wake kaimu mkurugenzi wa TGNP Bi. Grace Kiseru amesema TGNP imejipanga kuboresha mazingira yatakayomwezesha mtoto wa kike kupata elimu sawa na mtoto wa kiume. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.