}

WATU ZAIDI YA 70 WAMEPOTEZA MAISHA NDANI YA MASAA 72 KUFUATIA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI 16.

Maisha ya zaidi ya watu 70 yamekatishwa ghafla katika ajali za barabarani nchini Kenya katika muda wa masaa 72.

Maafisa wakuu serikalini na maafisa wa usalama barabarani wamelizuru eneo palipotokea ajali ya barabarani jana Jumanne, iliyoyahusisha magari 16 na zaidi ya watu 20 kupoteza maisha , katika eneo la Sachangwan kaunti ya Nakuru.

Katibu mkuu katika wizara ya uchukuzi na miundo mbinu John Mosonik, amesema serikali inajitahidi kutoa suluhuhisho la kudumu kusitisha maafa katika ajali hizo, mojawapo ya mikakati ikiwa ni kuundwa njia mbili kwenye eneo hilo zitakazotenganisha magari madogo na malori makubwa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.