}

ZAIDI YA THELUTHI MOJA YA SILAHA ZILIZOTUMIWA NA IS ZILITOKA KATIKA MATAIFA YA UMOJA WA ULAYA.

Utafiti mpya umebainisha kuwa zaidi ya theluthi moja ya silaha zilizotumiwa na kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiisilamu, IS nchini Iraq na Syria zilitoka katika mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Utafiti huo umebainisha kuwa silaha hizo zilitengenezwa nchini Bulgaria, Romania, Hungary na Ujerumani na nyingi zilinunuliwa na Marekani na Saudi Arabia ili kuyasaidia makundi ya waasi nchini Syria.

Ripoti ya utafiti huo pia imeonesha kuwa Urusi na China zilitengeneza zaidi ya nusu ya silaha zilizotumiwa na wanamgambo wa kundi la IS.

Wataalamu wa masuala ya silaha waliofanya utafiti huo walitumia miaka mitatu katika utafiti wao ukihusisha silaha kadhaa ikiwa ni pamoja na bunduki, risasi na vifaa vingine vinavyotumika kutengeneza milipuko.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.