}

WATU ZAIDI YA MILIONI 200 BARANI AFRIKA HATARINI KUPATA SARATANI YA INI.

 Na. Happy Shirima-Dar.

Inakadiriwa kuwa asilimia 30 ya wagonjwa wa saratani ya Ini wanapata tatizo hilo kutokana na matumizi ya aflatoksini (sumu kuvu)  kwenye vyakula ikiwemo mahindi ambayo hutumiwa na zaidi ya watu milioni 200 barani afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwenye warsha iliyoandaliwa na umoja wa afrika na taasisi nyingine kupitia program ya udhibiti wa aflatoksin  barani afrika (PACA) mkurugenzi wa  usalama wa chakula (TFDA) Raymond wigange amasemakuwa sera za vyakula bado hazijatoa kipaombele stahiki kwa tatizo hilo

Aidha ameongeza kuwa katika jitihada za kulinda afya za watu mataifa mbalimbali yanayoendelea yametunga sheria kudhibiti biashara ya vyakula vinavyoweza kuwa na aflatoksini ambapo pia vinachangia udumavu wa watoto.

Kwa upande wake mshauri wa masuala ya sumu kuvu kamisheni ya umoja wa Afrika prof Martin Kimanyi amesemakuwa warsha hiyo ambayo inafanyika desemba 4-5 mwaka huu inalenga kuhakikisha kuwa manufaa stahiki yanapatikana kutokana na mahindi Ambayo hutegemewa kama chakula kikuu na nchi 22 duniani kati ya hizo afrika ni nchi 16.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.