}

ATUPELE GREEN APIGWA CHINI SINGIDA UNITED DIRISHA DOGO.


Timu ya Singida United imetangaza rasmi kumuacha mchezaji wake Atupele Green katika dirisha dogo la usajili ambalo bado linaendelea.

Singida wameweka wazi hatua yao yakumuacha mchezaji huyo ambapo kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Instagram wameweka picha inayomuonesha Atupele nakuandika kuwa ameachwa.

Kabla yakuichezea Singida  United Atupele amewahi pia kuichezea JKT Ruvu kabla haijashuka daraja.

Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Novemba 15 na litafungwa Desemba 15 mwaka huu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.