}

TIRA YAZINDUA WARAKA MPYA MASHARTI YAKUFANYA BIASHARA.

Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini TIRA  imezindua waraka Na. 055/2017 ambao unahusu masharti ya kufanya biashara na makampuni ya bima mtawanyo, na madalali wa bima mtawanyo kutoka nje ya nchi ambao utaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2018.

Akuzungumza na waandishi wa habari kuhusu waraka huo, Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware amesema waraka huo ni sehemu ya jitihada za serikali kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kutokana na kupeleka biashara za bima nje ya nchi kupitia utaratibu ujulikanao kama mtawanyo.

Aidha Dkt Saqware amesem autekelezaji wa waraka huo utaimarisha kiwango cha tozo za bima zinzobakizwa hapa nchini hivyo kuongeza kiwango cha mchango wa sekta ya bima katika rasilimali fedha na uchumi wa ndani.
“Naomba itambulike kuwa utaratibu wa kupeleka biashara za bima nje ya nchi ni suala la kawaida katika masoko ya bima duniani, hivyo utaratibu huu unapofanyika vizuri huleta faida anuai kwa soko la ndani kama kushirikiana na makampuni ya bima ya nje katika kulipa hasara zitokanazo na majanga ya ndani ya nchi,
“Kuimarisha mapato na mitaji ya makampuni ya bima ya ndani, usimamizi mzuri wa madai, kuimarisha uwezi wa kitaalam na watendaji katika sekta ya bima nchini na kulinda mitaji ya makampuni ya bima nchini,”alisema Dkt. Saqware.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.