}

MSTAHIKI MEYA JIJI LA DAR KUHUDHURIA MKUTANO ADIS ABABA KUZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA VIONGOZI SERIKALI ZA MTAA.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili viongozi wa serikali za mitaa, mafanikio,na kujengeana uwezo kwenye utendaji kazi, mkutano ambao  utafanyika huko Addis Ababa.

Taarifa iliyotolewa leo Jijini dar es salaam kwenye vyombo vya habari imesema Mkutano huo utakuwa wa siku tatu na umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo Mameya wote.

Taarifa imeongeza kuwa Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na suala la bajeti katika halmashauri na ukusanyaji wa mapato ambapo Meya Mwita ataelezea changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam na namna ambavyo  kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.

Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali Duniani.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.