}

MKUU WA MAJESHI VENANCE MABEYO AJIPANGA UPYA SHAMBULIZI LA WANAJESHI KONGO.

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Venance Mabeyo amewahakikishia amani na kuwatoa hofu watanzania kufuatio vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania nchini Kongo. 

Akizungumza wakati wa kupokea miili ya wanajeshi hao Katika uwanja wa ndege wa Jeshi Mabeyo amesema hakuna hofu yoyote na sasa ni kujipanga upya kuhakikisha halitokei tena tukio baya Kama hilo ambalo ni lakwanza tangu kuanza kupeleka Jeshi nchini Kongo. 

Akizungumzia majeruhi na wanajeshi waliopotea baada ya shambulio amesema,  majeruhi wanaendelea vizuri na askari waliopotea wameonekana isipokuwa mmoja ambaye bado hajulikani alipo. 

"FDC ni kikundi kidogo Sana cha waasi ila wapo kimapigano zaidi nasisi tupo kule kiulinzi zaidi,  majeruhi wetu wanaendelea vizuri na wapo sehemu tofauti,  wengine wapo,  DRC, GOMA, KINSHASA, na Uganda. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.