}

HABARI YA JIWE LA TANI 20 LINALOCHEZA MKOANI MWANZA YAITIKISA DUNIA.

Mzee Makorokoro akilisukuma jiwe hilo kwa mguu na ndiye mwenye uwezo wakuliamuru jiwe hilo licheze. 
Nyaburebeka ni jina la jiwe kubwa linalopatika Kaskazini Magharibi mwa Tanzania katika kisiwa cha Ukerewe tarafa ya Ukara,mkoani Mwanza, kitu cha kushangaza au kuvutia ni kuwa jiwe hili linacheza.
Jiwe hilo huanza kucheza mara baada ya mtaalamu wa kulichezesha jiwe hilo kuanza kuliimbia na kuligusa kwa mkono au kulisukumwa na mguu mmoja.
Jiwe hili ambalo wataalamu wa kisayansi wanalikadiria kuwa na uzito zaidi ya tani 20 ,uzito ambao kwa nguvu ya mguu wa binadamu wa kawaida hauwezi kulisukuma .
Lakini hali ni tofauti kwa Mzee Kakuru Makorokoro na familia yake yote ambapo mpaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka kumi na miwili ana uwezo wa kulisukuma jiwe hilo likacheza au kutikisa.
Chanzo -BBC

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.