}

TFF- MFUMO WA USAJILI KWA NJIA YA MTANDAO UPO VIZURI.

Na. Anaseli stanley

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba mfumo wa usajili kwa njia mtandao kuanzia sasa umekaa sawa hivyo ni vyema vilabu husika vikakamilisha usajili wao kwa njia hiyo ya matandao hadi tarehe husika iliyopangwa na TFF ambayo ni tarehe 23 mwezi huu.

Akizungumza na kituochahabari.blogspot.com  afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Alfred lucas amesema kuwa mtandao huo ulisumbua siku ya mwisho ya ufungwaji wa dirisha dogo la usajili ambapo vilabu vilishindwa kuwasilisha majina ya wachezaji ambao wamesajiliwa katika kipindi hicho.

Lucas amesema wamefanya mawasiliano na wahusika CAF NA FIFA ambapo katika kila hatua wanayoipitia wamehakikisha nao wanaifahamu ambapo mpaka kufikia mapema hii leo mtandao huo umerudi katika hali yake ya kawaida.

dirisho dogo la usajili lilifunguliwa mnamo Novemba 15 na lilitarajiwa kufungwa desemba 15 lakini chngamoto ya mtandao limepelekea dirisha hilo kufungwa rasmi desemba 23 mwaka huu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.