}

ELIAS MAGULI ATOBOA SIRI KILIMANJARO STARS KUHARIBU MICHUANO YA CECAFA

Na. Anaseli Stanley Macha

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania bara,Elias Maguli amesema kwamba kikosi cha timu ya Kilimanjaro Stars kimeshindwa kufanya vizuri kwa kuwa hawakuwa na bahati ya kufanya vizuri katika msimu huu.

Maguli ameiambia Kituochahabariblospot kuwa pamoja na kuwa na wachezaji bora mwalimu mzuri lakini pia mchezo wa soka unahitaji bahati katika kupata matokeo ya ushindi baada ya dakika 90 kumalizika 

amesema kikosi cha kilimanjaro stars kipo katika kipindi cha mpito hivyo ni vyema watanzania kuendelea kuwapa ushirikiano ingawa imefanya vibaya lakini wanaamini katika michuano mingine wanaweza wakafanya vizuri zaidi.

kuhusu Mwalimu Ammy Ninje, Maguli amesema ni mwalimu mzuri japo watu wanamsema kuwa halijui soka la Tanzania lakini hawakumbuki kuwa ni mzaliwa wa Tanzania na amekulia hapa Tanzania jambo ambalo linamuweka katika nafasi nzuri ya kulitambua soka la Tanzania hivyo si vizuri kumhusisha katika kufanya vibaya kwa timu katika michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Mshambuliaji huyo Ameipongeza Zanzibar heroes kwa namna ambayo wamepambana na hata kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili ya michuano hiyo ambayo imemalizika jumapili iliyopita kwa Kenya kuibuka mabingwa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.