}

UONGOZI LIPULI FC WATAMBA KUFANYA USAJILI WA NGUVU DIRISHA DOGO.

Uongozi wa timu ya Lipuli Fc,umesema kwamba umekamilisha rasmi zoezi la usajili wa dirisha dogo lililofikia tamati siku ya Desemba 15 mwaka huu.

Mjumbe wa kamati ya ligi na mashindano wa klabu ya Lipuli FC,Haruna Salehe amesema kwamba zoezi hilo wamelikamilisha baada ya mfumo usajili kwa njia ya mtandao kurudi.

Aidha amesema kalbu hiyo imewasilisjha majina Saba ya wachezaji wapya ambao wamesajili katika kikosi hicho cha lipuli katika dirisha hili dogo la usajilia ambalo sasa linatarajiwa kufungwa tarehe 23 mwezi kutokana na mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao  kusumbua siku ya mwisho ya usajili kwa dirisha hilo.

Wachezaji ambao wamesajili na klabu hiyo yupo Jamali Simba Mnyate ambae amesajiliwa kwa mkopo,Adam Salamba,na wachezaji wawili kutoka ligi daraja la kwanza katika klabu ya Mufindi United, pia yupo Mghana kutoka katika klabu ya Mbao Fc ya Mwanza Ilemela.

Amesema wachezaji hao wamesajiliwa kulingana na matakwa ya ya benchi la ufundi la klabu hiyo linaloongozwa na kocha Suleiman Matola. 

Katika hatua nyingine Haruna Salehe amesema kikosi chote kipo mkoani Iringa na kinaendelea na mazoezi makali kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho ambapo wao wataumana dhidi ya Bukinafaso ya Morogoro

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.