}

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI DODOMA YAMPA DHAMANA MWENYEKITI UVCCM.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imempa dhamana Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge, visiwani Zanzibar Sadifa Juma Khamis .
Sadifa Juma Khamis alikamatwa nyumbani kwake mkoani Dodoma December 9 mwaka huu 2017 kwatuhuma za kuwapa vinjwaji wajumbe kutoka Kagera na kuwahaidi kuwalipia nauli ili wamchague mwenyekiti mpya wa UVCCM aliyekuwa akimpigia kampeni.
Mahakama imempa dhamana Sadifa Juma Khamis baada ya kujiridhisha kuwa hakuna shaka kwa mujibu wa sheria inayomzuia dhamana na kupewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja akiwa na bondi ya milioni moja.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.