}

MAGUFULI-WAZIRI WA FEDHA FUATILIA SUALA LA AIRTEL KUWA MALI YA TTCL.

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amezitaka mamlaka husika kutumia sheria zilizopo kuwabana wale wote ambao wanawapotosha Watanzania kwa kutoa takwimu za uongo.

Akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la ofisi ya taifa ya takwimu mjini Dodoma Rais Magufuli amesema kifungu cha sheria kinasema atakayepotosha takwimu adhabu ni kifungo cha kuanzia miezi sita hadi miaka mitatu au faini ya Millioni moja hadi millioni kumi au vyote kwa pamoja.

Rais Magufuli amevitaka vyombo vya habari na wataalam wa mitandao kuwaona wataaalm wanaohusika na takwimu ili kutoa takwimu sahihi na kumtaka Waziri wa fedha kufuatilia suala la Airtel kuwa ni mali ya TTCL kabla ya mwaka huu kuisha.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.