}

MAKAMBA AZINDUA KAMATI USHAURI WA MAZINGIRA DODOMA.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mh.January Makamba amezindua kamati ya kitaifa ya ushauri wa Mazingira mkoani Dodoma na kuzitaka Wizara mbalimbali kutoa taarifa ili kamati hiyo iwe na vitu vya kujadili.

Akizindua kamati hiyo Mh.Makamba amesema kwa mujibu wa sheria kamati hiyo itachunguza na kumshauri waziri au wizara yoyote ya kisekta kuhusu kulinda na kusimamia mazingira.

Mh.Makamba amesema serikali imefanikiwa kukabiliana na baadhi ya changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira unaotishia juhudi za serikali na wadau katika kufikia maendeleo endelevu na uchumi wa viwanda

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.