}

MBARAKA YUSUPH AREJEA BILA KUFANYIWA UPASUAJI JUU YA JERAHA LAKE.


Na. Anaseli Stanley Macha.


Mshambuliaji wa klabu ya Azam na timu ya taifa Tanzania Taifa stars Mbaraka Yusuph baada ya ya kupelekwa nchini afrika Kusini kwa ajili ya kuchekiwa hali ya goti lake baada ya kupata maumivu akiwa na timu ya Kilimanjaro stars amerejea  nchini.

Uongozi wa klabu ya Azam Fc kupita kwa msemaji wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga amesema mchezaji huyo amerejea baada ya kupata vipimo na hakuonekana na tatizo lolote zaidi ulikuwa ni mshuko wa kawaida

Jafari amebainisha kuwa Mbaraka kwa sasa anatarajia kujiunga na klabu yake ijumaa hii na ataanza mazoezi mepesi mepesi na januari mwakani atajiunga na wenzake kwa ajili ya kuitumikia klabu yake kwa michezo mbalimbali.

Aidha amesema vipimo vya Huku vilionesha Mbaraka ameumia katika meneo yake ya goti na anahitajika kufanyiwa upasuaji lakini vipimo vya Nchini Afrika kusini vimeonesha hakuna haja ya upasuaji kwana amepatwa na mshuko wa kawaida 

Mbaraka aliumia akiwa anaitumikia Kilimanjari Star katika michuano ya chalenji iliyomalizika hivi karibu nchini kenya.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.