}

AZAM IKO KAMILI KUIUA STAND KESHO

Azam Fc imethibitisha kukamilika katika kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Stand United mchezo utakaopigwa hapo kesho majira ya saa moja jioni katika uwanja wa chamazi jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga amesema kuwa kikosi chao kimekamilika na kimejiandaa vyema kuhakikisha kinapata alama Tatu hapo kesho.

Jafari amesema kocha amekiandaa kikosi na wanaamini kuwa wachezaji wote muhimu katika kikosi hicho wataanzaa ili kuona wanapata matokeo mapema .

'Tunaamini mchezo huo utakuwa mgumu sana lakini tuna kila sababu ya kutoka na ushindi'.alisema 


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.