}

MAKONDA AFANYA 'KUFURU' PUNGUZO LA BEI MLIMANI CITY, ASEMA NI ZAWADI YAKE KWA WANANCHI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametangaza Punguzo la Bei (Discount) la 70% kwa Bidhaa zote zinazopatikana Ndani ya Maduka Mlimani City kwa muda wa Wiki moja kuanzia Leo.

Punguzo hilo la bei ni kwa wananchi Wote ikiwa ni zawadi ya RC MAKONDA Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ili kuwapunguzia Wananchi makali ya Gharama.

MAKONDAamesema hayo kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza iliyopewa jina la DAR FRESHERS PARTY iliyofanyika Jana katika viwanja vya Parking ya Mlimani City

Kufuatia kufanikishwa kwa hafla hiyo Makonda amewashukuru wasanii mbalimbali wakiwemo WCB, AY, FID Q,  RUBY, KASSIM MGANGA, MWANA FA,  RAY C, LADY JAYDEE, MSAMI, CHRISTIAN BELLA, DULY SYKES na MRISHO MPOTO kwa kujitolea kutoa Burudani bila Malipo pamoja na vyombo vya Habari vilivyofanya jitihada za kufikisha taarifa za shughuli hiyo.

Amesema lengo la Tamasha hilo ni kujenga umoja kwa kuwakutanisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali kubadilishana mawazo  na kupatiwa maarifa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.