}

KADI NYEKUNDU YA POGBA YAMLIZA NIKKIWAPILI.



Msanii wa muziki wa Hiphop, mwanazuoni anayeunda kundi la weusi Nikkiwapili, ameonesha dhahiri mapenzi yake kwa klabu ya Mpira wa miguu ya Manchester United.

Nikki ameonesha mapenzi yake wakati timu hiyo iliposhuka dimbani Leo hii kukipiga na Arsenal na kufanikiwa kuwapiga washika bunduki goli tatu huku Arsenal wakiambulia goli Moja lakufutia machozi.

Licha ya ushindi huo Nikki alionesha kukasirishwa na maamuzi ya refa yakumzawadia kadi nyekundu mchezaji wao mahiri Paul Pogba, kiasi kilichopelekea kuingia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram nakuandika mapungufu ya refa , huku akisikitishwa zaidi nakutokuwepo uwanjani Pogba watakapokutana na Manchester City.

Kupitia Instagram Nikki ameandika "Refa kaamuwa kuwa beba man city kupitia mazishi ya arsenal imeniumaa sana kwanin pogba awakose city ahaaaa"

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.