}

MUIGIZAJI WA FILAMU BONGO, FLORAH MVUNGI KURATIBU SHINDANO MISS ROYAL COLLEGE.

Na.Geofrey Jacka.
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania Florah Mvungi, yupo kwenye maandalizi ya shindano la kumtafuta mrimbwende na mtanashati wa Chuo Cha Royal jijini Dar es salam.

Akizungumza na kituochahabari.blogspot.com Florah amesema, wapo katika hatua za mwisho za maandalizi na wamepanga Shindano hilo lifanyike tar 22 Desemba mwaka huu.
"Maandalizi yapo vizuri, na washiriki wamejitokeza tayari, upande wa mamiss wapo wanne, Sophia, Jack, Romana na Rehema na mamista wapo watano Abel, Samson, Nathan, Reward na Abel King" alisema Florah.
Akizungumzia burudani Florah amewahakikishia watakaohudhuria kuwa itakuwa ni bonge moja la shindano ambalo halijawahi kufanyika katika vyuo vya Dar wala mikoani.
"Unajua nini, mi nashauri watu wafike tu siku ya tukio, kwa jina langu lilivyokubwa siwezi kuandaa shindano bovu nikajivunjia heshima yangu. Kwanza shindano litakuwa Live TVE , kutakuwa na Red carpet, Opening dance, Fashion show pia tutamtafuta Photogenic wakike, warembo hao sio wakitoto nakuambia" alijigamba Florah.
Mavazi yatakayovaliwa na warembo katika shindano ni, vazi la ufukweni, vazi la ubunifu, vazi la kawaida na vazi la usiku.

"Shindano litafanyika JM night club Manzese, najua wengi wanapafahamu, tutaburudika mpaka asubuh, mi mwenyewe kuna saplaiz nimewaandali siku hiyo ukumbini, chamsingi watu wajae tuu." alimalizia Florah.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.