}

DCI ROBERT BOAZ ATOA TAKWIMU ZAKIUSALAMA KIPINDI CHA JANUARY MPAKA NOVEMBA.

Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI ispekta jenerali Robart Boazi amesema hali ya usalama nchini inaridhisha katika kipindi cha januari hadi novemba mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu hali ya usalama nchini Ispekta Boazi amesema kipindi cha mwezi january hadi novemba 2016 makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa yalikuwa ni elfu 68204 ikilinganishwa na makosa elfu 61794 mwaka 2017.

Ispekta Boazi amesema makosa ya ubakaji na unajisi yameongezeka kwa asilimi 63,makosa ya uhalifu wa kifedha yamepungua kwa asilimi 18.0 na makosa ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 42.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.