}

ASILIMIA 80 YA WAKULIMA HAWANUFAIKI NA KILIMO WANACHOKITEGEMEA




Utafiti uliofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya MIICO  na NADO Katika wilaya za Wanging'ombe,Mbozi na Kyela umebaini zaidi ya asilimia 80 ya wakulima hawanufaiki na sekta ya kilimo ambacho wanakitegemea katika maisha yao ya kila siku.

Aidha imebainika kwamba asilimia 47 ya wakulima wa zao la Mahindi wanapata faida kidogo ya mazao ikilinganishwa na Gharama zinazotumika katika uzalishaji wake.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Miico Bwana Adam Msimingwa katika uwasilishaji wa Utafiti huo kwa wadau wa kilimo wilayani Wangingombe wakiwemo wakulima,Madiwani na viongozi wengine wa Serikali.

Kwa Mujibu wa Hesabu ya Wakulima Katika Kilimo Cha Ekari Moja Kwa Kupata Gunia 26 na Kuuzwa Kwa Zaidi ya Shilingi  Laki Sita  Kati ya Zaidi ya Laki Tano Kama Gharama za Uendeshaji Kilimo Imeonekana Mkulima Anapata Faida ya Shilingi elfu 39 Kwa Kipindi Cha Miezi Sita Fedha Ambayo Bado Imekuwa ni Hasara Kubwa Ukilinganisha na Muda.

Kutokana na Takwimu Hizo Baadhi ya Wakulima Wananyanyuka na Kupaza Sauti Zao Mbele ya Viongozi Mbalimbali wa Serikali Wakitaka Zao la Mahindi Litambulike Kama Mazao Mengine ya Korosho Yenye Usimamizi Mkubwa Kupitia Bodi.



Ally Kassinge ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe ametumia Fursa Hiyo Kupiga Marufuku Walanguzi wa Mahindi Kuingia Kufanya Kazi Hizo Bila Msimu wa Ununuzi Kutangazwa na Yeye na Kwamba Atakaye Kiuka Maagizo Hayo Kuanzia Msimu wa Kilimo Ujao Atakamatwa Kama Mwizi Anayewaibia Wakulima.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.