}

BALOZI WA MAREKANI KATIKA UMOJA WA MATAIFA ATOA ONYO AZIMIO LINALOUKOSOA UAMUZI WA TRUMP.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, ametoa waraka wa onyo kuwa Marekani itachukuwa orodha ya majina wakati wa kupiga kura kuhusu azimio linaloukosoa uamuzi wa Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Hailey ametoa onyo hilo kwenye mtandao wake wa Twitter na kuandika kuwa uamuzi wa Trump ni takwa la umma wa Marekani la wapi uwepo ubalozi wao na kusisitiza kuwa itaorodhesha majina ya wale wote watakaopiga kura kuikosoa.

Pendekezo hilo la kuikosoa Marekani kwa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel limewasilishwa mbele ya Baraza kuu la Umoja wa mataifa na Misri ikiungwa mkono na Nchi za Kiarabu na za Kiislamu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.