}

CHINA IMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA MIRADI YENYE KIPAUMBELE.

China imeahidi kushirikiana na Tanzania kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

Hayo yameelezwa mjini Beijing na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming pamoja na  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC) Bw. Ning Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Miradi hiyo ni pamoja na kuendeleza nishati ya umeme ambapo Serikali imedhamiria kuzalisha umeme wa megawati 5000 ifikapo mwaka 2020 ili kuharakisha utekelezaji wa agenda ya uchumi wa viwanda ambao unahitaji umeme wa kutosha na wauhakika.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.