}

WAZIRI JAFO WA TAMISEMI AZINDUA KAMPENI YA "MKOA WETU VIWANDA VYETU".

Waziri wa TAMISEMI Mh. Seleman Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo leo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini,
Akizungumza katika uzinduzi huo Mjini Dodoma Mhe. Jafo amesema kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda hivyo TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya uendelezaji viwanda katika Ofisi zote za SIDO Mikoani.
Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa wetu viwanda vyetu itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.