}

MNADA NYUMBA ZA LUGUMI WAMLAZA SENTRO BILIONEA.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, SACP Mambosasa.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia  Dk. Louis Shika ambaye ameshinda mnada wa ununuzi wa nyumba za Said Lugumi na baada ya kubaini kuwa alitumwa na Lugumi mwenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi kutokana na mazingira ya tukio husika.

Kamanda Mambosasa amesema Ingawa hana vielelezo vya  kuthibitisha suala hilo, lakini muonekano wa mnunuzi huyo ulikuwa unatia shaka na kwamba Jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi

Dk. Louis Shika ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo cha polisi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.