ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI.
Serikali imeshauriwa kuwaongeza Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ili kuweza kumsaidia Mkulima aweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi .
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo (ANSAF),Audax Rukonge wakati wa Mkutano uliowashirikisha wadau mbali mbali wa Kilimo AMBAPO amesema kumtumia Afisa Mgani mmoja katika Kijiji kimoja hakuna tija wala msaada wowote kwa mkulima.
Aidha amesema kuwa kutokana na hali ilivyo ya uchache wa Maafisa Ugani kuna haja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya Ugani kwa Wakulima ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika.
Naye Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine (SUA) Dk Sizya Lugeye, ameitaka serikali Kuhakikisha wanawaongezea nguvu maafisa Ugani waliopo ikiwemo kuwapata fedha pamoja vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanizi zaidi katika kuwahudumia wakulima ili kukuza secta ya kilimo nchini
No comments