}

NAIBU WAZIRI TAMISEMI JOSEPH KAKUNDA ATOBOA SIRI MFUMO MPYA WA ELIMU.

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda.
Serikali inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo hutolewa kwa miaka 7.

Akitoa ufafanui juu ya watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda amesema  mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.


Aidha Mh. Kakunda amesema kutokana na mfumo huo mpya ambao utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa kuolewa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.