}

MAHAKAMA YAITUPILIA MBALI KESI ILIYOKUWA INAKABILI MWANAMUZIKI DIAMOND

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Diamond Platnum.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 10/2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo.

Hakimu Devotha alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.

Katika pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakamani hapo anadai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Awali Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine alikuwa anaomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond. Mwanamitindo huyo alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiiomba mambo mbalimbali likiwemo la matunzo ya mtoto waliozaa na msanii huyo.

Katika kesi hiyo, Hamisa anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi. Hamisa alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Hata hivyo, Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Diamond akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi sh. milioni tano kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.