}

UPASUAJ WA KUREJESHA VIUNGO WAENDELEA AGAKHAN.


Hospitali ya Aga Kan kwa kushilikiana na Taasisi ya women for women na Hospitali ya Taifa Muhimbili leo  wameendelea  kufanya upasuaji wa kurudisha viungo vilivyotolewa katika mwili wa binadamu kutokana na ugonjwa wa saratani ikiwemo Matiti.

Akizungumza jijini Dar es salam Daktari bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Aga Kan Aidan Njau amesema kwa Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika kwa upasuaji wa kumuwekea mwanamke titi ambapo tayari wanawake wawili wamejitokeza kufanyiwa upasuaji huo.


Naye Daktari bingwa wa upasuaji kutoka  hospitali ya Taifa Muhimbili Edwin Mrema amesema zoezi hilo ni mwendelezo wa kampeni ya kuwasaidia kinamama na watoto ambao waliondolewa viongo vyao kwa kuungua na moto  au kuugua saratani kurejea katika hali yao ya kawaida.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.