}

Health summit kuandaa kongamano la Afya.


Taasisi ya Tanzania Health Summit wanatarajia kuandaa kongamano la kitaifa la afya litakalofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalim Julius kambarage Nyerere tarehe 14-15 November, 2017 lengo kuu likiwa ni kuchangia juhudi za serikali katika kuboresha afya kwa kujadiliana changamoto zinazokabili sekta ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Raisi wa mkutano wa Tanzania Health Summit  Dr,Omary Chillo amesema kuwa kamati ya maandalizi inaundwa na taasisi saba zikiwemo  Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, wizara ya afya ya serikali ya mapinduzi Zanzibar, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), APHTA, Christian Social Services Commission, baraza kuu la waisilam Tanzania na Tindwa Medical and Health Services kwa lengo la kuunga juhudi za awam ya tano ya kuleta maendeleo kwa jamii na uchumi wa viwanda.

Aidha, Katibu wa Tanzania Health Summit Dr, Rebecca John ametoa wito kwa wadau wa afya kutoka serikalini na mashirika binafsi, mahospitali,  na asasi zisizo za serikali kushiriki kikamilifu katika mkutano wa mwaka huu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.