Haya ndio yaliyojiri kwenye soko la hisa DSE.
Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 3 Novemba 2017.
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Shilingi Billioni 20 ya wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017 hadi Shilingi Bilioni 3 kwa wiki iliyoishia 3 Novemba 2017.
Hata ivyo Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa Mil 1.6 ya wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017 hadi hisa Mil 3.5 ya wiki iliyoishia 3 Novemba 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TCC……………………………………………41%
TBL……………………………………………27%
CRDB………………………………………….16%
VODA………………………………………….11%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Shilingi Bilioni 217 kutoka Shilingi Trilioni 20.5 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyoishia tarehe 3 Novemba 2017. Punguzo hilo limetokana na kupungua kwa bei za hisa za KA (8%), JHL (8%), CRDB (6%) na TBL (5%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kwa Shilingi Bilioni 112 kutoka Trilioni 10.163 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.051 wiki hii. Hii ni kutokana na kupungua kwa bei ya hisa za CRDB (6%) na TBL (5%).
Kampuni
|
3 November 2017 (Shilingi)
|
27 October 2017 (Shilingi)
|
Badiliko (%)
| ||||
CRDB
|
-5.88%
| ||||||
DCB
|
0.00%
| ||||||
DSE PLC
|
1,220
|
1.67%
| |||||
MBP
|
0.00%
| ||||||
MCB
|
0.00%
| ||||||
MKCB
|
0.00%
| ||||||
MUCOBA
|
0.00%
| ||||||
NMB
|
2,750
|
0.00%
| |||||
PAL
|
0.00%
| ||||||
SWALA
|
0.00%
| ||||||
SWIS
|
3,500
|
0.00%
| |||||
TBL
|
13,200
|
1
|
-5.04%
| ||||
TCC
|
16,800
|
1
|
7.69%
| ||||
TCCL
|
1,200
|
0.00%
| |||||
TOL
|
0.00%
| ||||||
TPCC
|
1,520
|
0.00%
| |||||
TTP
|
600
|
0.00%
| |||||
VODA
|
0.00%
| ||||||
YETU
|
0.00%
| ||||||
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine
| |||||||
ACA
|
5,430
|
-0.55%
| |||||
EABL
|
5,290
|
-0.38%
| |||||
JHL
|
9,680
|
1
|
-7.72%
| ||||
KA
|
-8.33%
| ||||||
KCB
|
0.00%
| ||||||
NMG
|
2,360
|
-0.84%
| |||||
USL
|
0.00%
| ||||||
Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
|
20,237
|
2
|
-1.07%
| ||||
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
|
10,051
|
1
|
-1.10%
| ||||
Kiashiria cha DSEI (pointi)
|
2,101
|
-1.08%
| |||||
Kiashiria cha TSI (pointi)
|
3,834
|
-1.08%
|
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 23 kutoka pointi 2,124 hadi 2,101 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Kenya Airways (KA), Jubilee holdings Ltd (JHL), CRDB BANK (CRDB) na Tanzania Breweries Ltd (TBL).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepungua kwa pointi 43 kutoka pointi 3,876 hadi pointi 3,833 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za CRDB na TBL.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepungua kwa pointi 77 kutoka pointi 5,379 hadi pointi 5,303
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) kimeshuka kwa pointi 33 kutpka pointi 2,497 hadi pointi 2,464.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 3 Novemba 2017 yalikuwa Shilingi Bilioni 15.7 kutoka Shilingi Milioni 500 wiki iliyopita ya 27 Oktoba 2017
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na moja (11) za serikali na pia za makampuni binafsi zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 17.4 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 15.7
No comments