}

MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUKABILIANA CHANGAMOTO ZA MAKUZI YA WATOTO KUANZA RASMI KESHO.

Mkurugenzi wa kinga za watoto wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto akizungumza na waandish wa habari jijini dar es salaam  wakati akifungua mkutano wa kimataifa ulioandaliwa kwa ushirikiano wa aga kan foundation, unicef, who, pac na ti ambao una lengo la kujadili maendeleo ya uwekezaji kwa maisha ya watoto.(Picha.Anaseli Stanley Macha)
Mkurugenzi wa kinga za watoto wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dkt. neema rusibamayila amefungua mkutano wa kimataifa uliowakutanisha mashirika na taasis zinazojihusisha na masuala ya watoto dunia ambapo mkutano huo una lengo la kujadili uwekezaji na namna mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za makuzi ya watoto.
Wataalamu kutoka mataifa 44 dunian ambao wamewasili hapa nchn kwa lengo la kushirki mkutano wa kimataifa wa kujadili uwekezaji kwa maisha watoto wachanga na namna kukabilia na changamozo za makuzi ya mtoto, utakaofanyika serena hoteli kuanzia kesho jumanne hadi alhamic wiki hii.(Picha.Anaseli Stanley Macha)
Akizungumza katika ufunguzi huo dkt rusibamayila amesema watapokea mapendekezo ambayo yatatokana na majadiliano katka mkutano huo kwa lengo la kuboresha mahitaji ya mtoto ingawa pserikali tayari imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali katka kuhakikisha wanasaidia malezi ya watoto kulingana na mahitaji ya ukuaji wake.
Mratibu wa maendeleo ya kibinadamu wa aga kan foundation LEONARD CHUMO ALEX. (Picha.Anaseli Stanley Macha)
Mkutano ambao umeandaliwa kwa ushirkiano wa taasisi ya maendeleo ya binadamu ya aga kan. unicef, who shirika la PAC  na TI unatarajiwa kuanza rasmi kesho jumanne mpka alhamic wiki hii.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.