}

Nape amjia juu Nyalandu kuihama CCM.

Na.Geofrey Jacka.

Picha aliyoitumia Mh.Nape kwenye ukurasa wake wa Instagram kuelezea hisia zake juu ya kujiuzulu kwa Nyalandu. (Kushoto Nape Nnauye, katikati Lazaro Nyalandu na kulia ni katibu mkuu wa CCM Abdurahman Kinana.)

Aliyekuwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye, amevunja ukimya baada ya kujitokeza kuongelea sakata la kujivua Ubunge na kujivua uanachama wa CCM kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.

Nape amejitokeza ikiwa bado vuguvugu la sakata hilo na mijadala ikiendelea kuhusu kujiuzulu kwa Nyalandu nyazifa mbalimbali alizokuwa nazo ndani ya chama cha mapinduzi huku akiifananisha hatua ya Nyalandu ni sawa na kubadili Imani kienyeji, hatua ambayo yeye binafsi hawezi kuichukua.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Nape ameandika "Chama cha Siasa ni Itikadi, Itikadi ni Imani. Siamini sana katika Kubadili Imani KIENYEJI. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani sio nje."

Aidha nape amewashangaa waliodhani kuwa ataihama CCM ambapo kupitia uwanja wa maoni wa mtandao huo ameanza kuwashukuru wanaomuunga mkono katika mtizamo wake, huku akimalizia kwa sentensi iliyotafsiriwa na baadhi ya watu kuwa huenda ana mgogoro na aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania ambaye alijiuzulu na baadae kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mh. Edward Lowasa.

"Nimesoma comments nyingi sana leo, nawashukuru sana. Nawashukuru mnaoniunga mkono kwenye mtizamo wangu, na hii haina maana kuwa wasiowaza kama sisi ni maadui na wala hatupuuzi hoja zao. Lakini hivi nikweli kwamba kuna watu walidhani kwa dhati naweza kwenda kukaa chama kimoja na Mzee wangu EL???!!!!!????????!!!!!!!!!" alisema Nape.

Nyalanda amejuzulu Ubunge baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka 17 mfululizo tangu alipochaguliwa kwa Mara ya kwanza mnamo mwaka 2000,. Pia amewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.