}

TSNP-SERIKALI ITOE TAMKO WANAFUNZI ELFU 31 WALIOKOSA MKOPO.


Na. Happy Shirima.



TAASASI isiyo ya kiserikali (TSNP) imeiomba Serikali kutoa tamko kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu waliokosa mikopo elfu 31 na kushindwa kuendelea na masomo wakati wamekidhi  vigezo.

Ombi hili limetolewa jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa idara ya haki na Wajibu wa Taasisi hiyo, Abdul Nondo,kufuatia tamko lililotolewa na Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako, ikielezea kua adhama ya Serikali imetimia kwa kuwapatia mikopo wanafunzi elfu 30.

Amesema kuwa,wanafunzi hao wamekosa mikopo kutokana na bajeti iliopitishwa na Serikali kwa mwaka 2017/18 shiling billion 427 ambapo shiling billion 108.8 ni kwa ajili ya wanafunzi elfu 30 tu katika ya wanafunzi efluhusiano 61 walioomba kwa mwaka wa kwanza.

Ameongeza kuwa, endapo Serikali ama wizara husika haitotolea ufafanuzi kuhusu wanafunzi waliokidhi vigezo na kukosa mkopo ndani ya siku tano basi wanaadhimia kutoa tamko kwa wanafunzi na marais wa vyuo  nchi nzima. 


Kwa upande wake, Aziza Rashid ambae ni mwanafundi wa chuo cha biashara  (CBE) mwaka wa kwanza amesema kuwa,amefikia hatua ya kueka vyeti vyake bondi kwa ajili ya kupata mkopo ili aweze kusoma baadq ya kupata chuo na kufika chuo akakosa mkopo.

"Nimeeka vyeti bondi vyeti vyangu ili niwaze kupata mkopo niendelee na masomo mwaka wa kwanza nikijua mara hii nitaweza kupata mkopo kutokana na kua mwaka jana nilikua nimekidhi vigezo na nikakosa,sasa naomba Serikali ituambie nini hatma yetu kwani usajili unakaribia kuisha na tunataka kuendelea na masomo "alisema Aziza. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.