}

TAASISI ZA UTAFITI SEKTA YA KILIMO ONGEZENI UFANISI- WAZIRI MTIGUMWE.

Na Mathias Canal, Arusha.

Waziri wa Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe (katikati)

Taasisi za utafiti katika sekta ya kilimo zimetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha wakulima kote nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika ipasavyo.

Wataalamu wa utafiti wamepaswa kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti  ikiwemo Kuongeza ujuzi katika Utafiti wa mazao mbalimbali wasiishie katika zao moja au mawili tu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe alipotembelea Taasisi ya Utafiti ya viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Tropiki iliyoanzishwa mwaka 1945 yenye jukumu la kuendeleza utafiti na kutoa huduma za matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, Taasisi ya utafiti na Mafunzo ya Tengeru, HORTI Tengeru iliyoanzishwa mwaka 1980 sambamba na Kituo cha Utafiti wa kilimo na Maendeleo Selian (SARI) kilichofunguliwa mwaka 1979 kama shamba la utafiti wa ngano na Shayiri chini ya ufadhili wa Canada.

Mhandisi Mtugumwe aliwasihi watafiti hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani bajeti ya serikali pekee haiwezi kutosha.

Alisema wataalamu hao wanapaswa kufanya tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema Wizara ya kilimo ipo tayari kuwakaribisha baadhi ya watafiti kwenye kamati ya Bunge inayoshughulikia kilimo ili kuwasilisha vitu walivyovifanya katika Utafiti mbele ya wabunge ambaomoja ya jukumu lao kubwa ni kutunga sheria.

Kuhusu changamoto za nyumba za wafanyakazi alisema kuwa tayari zipo katika Taasisi na vyuo vyote vya Utafiti hivyo itakapofanywa tathmini yote kwa ajili ya vyuo vya kilimo nchini litatekelezwa pia katika chuo hicho.

Mhandisi Mtigumwe alisema watafiti hao wanapaswaKuwa na mikakati ya kupata vijana wengi zaidi ili waweze kujifunza fani hiyo kuhusu Utafiti kwani bado serikali inatambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.

Kuhusu mpango wa Wizara ya Kilimo kwenye Mazao ya mboga mboga na matunda alisema kuwa ni sehemu ya kipaumbele cha Wizara na serikali huku akiahidi kuwasaidia kutengeneza kitalu nyumba (Green House) .

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.