}

STARS IMEREJEA USIKU WA KUAMKIA

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imerejea usiku wa kuamkia leo hii kikitokea nchini Benin ilienda  kushiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Benin.

Alfred Lucas Afisa Habari wa TFF, alisema baada ya timu hiyo  kuwasili hapa nchini baadhi ya wachezaji wameelekea kambini katika vilabu vyao huku wekingine wameelekea majumbani mwao kabla ya kuungana na timu zao kwa ajili ya kushiriki michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Lucas alisema  kwa wachezaji wa Simba na Prisons wao moja kwa moja TFF iliamua kuwasafirisha mapema ili wakajiunge na timu zao kutokana na makubaliano ambayo wamekubaliana na viongozi wao.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.