}

LIPULI YAENDELEA NA MAZOEZI YA KUWAVAA SINGIDA UNITED

Kikosi cha lipuli kimeendelea na mazoezi ya kujiwinda dhidi ya walima Alizet wa singida Singida United 

Akizungumza na kituo cha Habari Leo Kocha msaidizi wa timu Hiyo Amri Said amesema maandalizi kuelekea katika mchezo huo ambao watakuwa ugenini kwa upande wao yamekamilika.

Amesema wachezaji wana hali nzuri na wako tayari kupambana katika mchezo huo ili kutoka na ushindi ambao ndio utakuwa faida kwao.

koacha Said amesema wanaiheshimu sana Singida united lakini watacheza kwa tahadhali kubwa kuhakikisha wanapata ushindi ama sare lakini si kupoteza mchezo huo

Singida United inatarajia kuwakaribisha lipuli kutoka Iringa siku ya jumamosi katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa katika uwanja wa namfua uliopo Mjini Singida.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.