}

MASHABIKI YANGA TUTAMPOKEA MO,IBRAHIMU KWA MIKONO MIWILI


Na, Anaseli Stanley 0717351469

kuelekea katika kufunguliwa kwa dilisha dogo la usajili mshabiki wa Yanga wamesema wako tayari kumpokea kwa mikono miwili  mchezaji kiungo wa klabu ya wekundu wa msimbazi simba Mohamed Ibrahimu endapo uongozi wa klabu ya yanga utakubaliana kumsajili mchezaji huyo.

Waziri Jitu mwenyekiti wa tawi la Yanga la Umoja Tandale kwa Mtogole amesema simba wameshindwa kumtumia vizuri kiungo huyo  hivyo ni vyema akajiunga na yanga na wao wako tayari kumpokea.

Jitu ameongeza kwa kumsifia uwezo alionao mchezaji  Mohamed Ibrahimu katika nafasi za kufunga hata kuasidia kupandisha timu kwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na anashangaa kuona simba wakimuacha benchi.

amesema awezi kuwalazimisha uongozi au kamati ya usajili katika kumsajili lakini anaona kuna kila sababu ya yanga kukamilisha usajili wa kiungo huo kwana atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chao.

Mohamedi Ibrahimu hivi karibuni kumekuwa na taarifa tofauti juu ya mchezaji huyo ambazo zinamuonesha kuwa huenda akajiunga na mabingwa watetezi Yanga kutokana na kuwa mkataba wake na klabu ya simba unaelekea ukingoni.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.