}

LWANDAMINA SAJILI MBADALA WA NGOMA, NGOMA HANA FAIDA KWA SASA


Na. Anaseli Stanley. 0717351469


Mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuingia katika usajili ili kuongeza nguvu katika kikosi chao kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye kikosi hicho hasa katika eneo la ushambuliaji ambapo mchezaji wa kimataifa mzimbabwe Donald Ngoma ameonekana kutokuwa na faida katika kipindi hiki.

akizungumza na kituo cha habari leo mwenyekiti wa tawi la Yanga  la umoja Tandale kwa Mtogole Waziri Jitu amesema wao wanampa nafasi Mwalimu Geogre Lwandamina kutazama mapungufu yaliyomo kwenye kikosi hicho na kulitumia vyema Dirisha dogo la usajili ambalo linafungulia hapo kesho.

Jitu amesema mpaka sasa Mshambuliaji Mzimbabwe hana faida katika kikosi hicho ni vyema mwalimu akasajili wachezaji ambao watachukua nafasi yake ili kuisaidia yanga katika michuano ya kimataifa.

aidha amewataja wachezaji kama Abdalah Rashidi wa Tanzania Prisons na Ditram Nchimbi wa Njombe Mji wanaweza kuwa wachezaji watakaoisaidia yanga katika michezao mbalimbali ya ndani na hata nje kwani uwezo wao ni mkubwa na wanauweza kuchezea kunako klabu ya yanga.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.