}

Mkuu wa mkoa Geita aipongeza Halmashauri.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo.  

" Inashangaza sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya Serikali"Alisema Lughumbi.

Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.